Utapiamlo ni ugonjwa
unaoathiri kukua kwa mwili na akili ya mtoto. Idadi ya watoto wanaopata ugonjwa
huo hapa nchini inakadiriwa kuwa asilimia 42 huku ikiwa inahofiwa kuongezeka
ambapo mara nyingi huwapata watoto wenye umri chini ya miaka 18.
Kwa nini ni vigumu sana kushinda
tatizo hilo? Ili kupata jibu, ni vyema kuujuwa kwanza ugonjwa wa utapiamlo, na
kuchunguza athari na visababishi vilivyotia mizizi vya ugonjwa huo.
UTAPIAMLO HUSABABISHWA NA NINI?
Utapiamlo husababishwa na ukosefu wa
vitamini na madini ya kutosha katika chembe za mwili, na kwa kawaida
husababishwa na mambo mawili:
- Ukosefu wa protini, nishati, vitamini, na madini.
- Maambukizo ya mara kwa mara.
Magonjwa kama vile kuharisha, surua,
malaria, na magonjwa ya kupumua hudhoofisha mwili sana na kupunguza vitamini na
madini. Magonjwa hayo humfanya mgonjwa apoteze hamu ya kula naye hula chakula
kidogo sana, na hivyo anapata utapiamlo. Kwa upande mwingine, mtoto asiyepata
chakula cha kutosha anaweza kuambukizwa magonjwa kwa urahisi. Jambo hilo
huongeza idadi ya watoto wanaokufa kwa sababu ya kukosa vyakula vinavyojenga
mwili.
KWA
NINI UTAPIAMLO UNAWASHAMBULIA ZAIDI WATOTO ?
Watoto wanakua haraka na hivyo
wanahitaji nishati na protini nyingi zaidi. Vivyo hivyo, akina mama wajawazito
na wanaonyonyesha wanaweza kupata utapiamlo.
Mara nyingi, mtoto mchanga huanza
kuathiriwa akiwa tumboni. Ikiwa mama hapati chakula cha kutosha au hali chakula
bora kabla na wakati wa mimba, basi atajifungua mtoto mwenye uzito kidogo.
Mtoto huyo akiachishwa kunyonya mapema, asipolishwa vizuri, au usafi
usipozingatiwa, anaweza kuugua utapiamlo.
Mtoto hawezi kukua au kusitawi
vizuri asipopata vitamini na madini muhimu. Yeye hulia bila sababu yoyote na
kuwa mgonjwa-mgonjwa. Kadiri hali yake inavyozorota ndivyo anavyozidi kukonda,
macho na utosi wa kichwa hubonyea, ngozi na tishu za mwili hukauka, na uwezo wa
kudhibiti joto la mwili hupungua.
Utapiamlo humwathiri mtoto kwa njia
nyingine ambazo pia zinaweza kuathiri ukuzi wake. Kwa mfano, kutopata madini ya
kutosha hasa chuma, iodini, na zinki na vitamini hasa vitamini A - kunaweza
kusababisha madhara hayo.
MADHARA MABAYA ZAIDI
Utapiamlo hudhuru kabisa mwili, hasa
mwili wa mtoto. Unaweza kudhuru viungo na mifumo yote mwilini kutia ndani moyo,
mafigo, tumbo, matumbo, mapafu, na ubongo.
Uchunguzi mbalimbali umeonyesha
kwamba ukuzi wa polepole wa mtoto hudhoofisha maendeleo yake ya kiakili na
uwezo wa kufikiri na kufanya vyema shuleni.
Mtoto anaweza kuendelea kuathiriwa
na matokeo ya utapiamlo hata anapokuwa mtu mzima.
VISABABISHI
Kama ilivyotajwa awali, utapiamlo
husababishwa na ukosefu wa chakula. Lakini, unasababishwa pia na mambo mengine
mazito zaidi ya kijamii, kiuchumi, kitamaduni, na ya kimazingira. Kisababishi
kikuu ni umaskini, ambao huathiri mamilioni ya watu, hasa katika nchi
zinazoendelea. Hata hivyo, mbali na kuwa kisababishi, umaskini pia husababishwa
na utapiamlo. Ukosefu wa chakula cha kutosha hupunguza uwezo wa kufanya
kazi, na hilo huzidisha umaskini.
KUTIBU NA KUZUIA
Mtoto mwenye utapiamlo anaweza
kutibiwaje?
Ikiwa mtoto huyo amedhoofika kabisa
huenda ikafaa alazwe hospitalini kwanza
Katika hatua ya pili, mtoto
hunyonyeshwa na kusaidiwa ale chakula kingi iwezekanavyo. Ni muhimu kuboresha
tena hali yake ya kihisia na ya kimwili wakati huo. Mtoto huyo anaweza kukua
vyema akitunzwa kwa uangalifu na kuonyeshwa upendo. Wakati huo huenda ikafaa
kumfundisha mama kumtunza mtoto wake kwa kumlisha chakula kinachofaa na kutunza
afya yake ili asipate tena utapiamlo. Kisha mtoto hurudishwa
nyumbani. Ni muhimu mtoto apelekwe hospitalini au kwenye kliniki ili maendeleo
yake yachunguzwe.
Hata hivyo, kuuzuia utapiamlo ndilo
jambo la maana zaidi. Ndiyo sababu serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali
katika nchi nyingi yameanzisha miradi ya kuboresha chakula kinacholiwa na umma.
Jamii pia hujitahidi kuzuia utapiamlo kwa njia nyingi, kama vile kuanzisha
mipango ya kuwaelimisha watu kuhusu chakula, kuwa na maji safi ya kunywa,
kujenga vyoo, kudumisha usafi wa mazingira, kutoa michango kwa ajili ya kampeni
za chanjo, na kusimamia ukuzi na maendeleo ya watoto.
Lakini mtu mmoja-mmoja anaweza
kufanya nini ili kuzuia utapiamlo Lakini pia mama anashauriwa kirudi hospitali
kumwona tena daktari wa watoto au kurudi hospitalini siku saba baada ya
kujifungua, mtoto anapokuwa na umri wa mwezi mmoja, na kila mwezi baada ya
hapo. Mama anapaswa pia kumwona daktari mtoto anapokuwa na dalili za
kupungukiwa na maji mwilini, anaharisha sana, au akiwa na dalili za homa.
No comments:
Post a Comment